​Rayvanny Nyimbo Mpya 2026 MP3 Download - Zilizovuma Mpya

Nyimbo Mpya Wiki Hii

Rayvanny Biography

Rayvanny Biography

Raymond Shaban Mwakyusa, anayejulikana zaidi kwa jina la kisanaa la Rayvanny (au Chui), ni mmoja wa wasanii wakubwa, wenye vipaji vya hali ya juu vya uandishi na uimbaji wa muziki wa Bongo Flava, Afro-pop, na Amapiano nchini Tanzania na kimataifa. Yeye ndiye Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa lebo ya muziki ya Next Level Music (NLM), inayowasimamia wasanii kama Macvoice. Na kusslove

Early Life and Background

Rayvanny alizaliwa tarehe 22 Agosti 1993 Mkoani Mbeya, Tanzania. Alianzia safari yake ya muziki tangu akiwa shuleni ambapo mwaka 2011 alishinda shindano la FreeStyle rap la Tip Top Connection jijini Dar es Salaam kabla ya kujikita zaidi kwenye uimbaji na uandishi wa nyimbo.

Music Career and Breakthrough

Alipata mafanikio makubwa mwaka 2016 baada ya kusainiwa chini ya lebo ya WCB Wasafi inayoongozwa na Diamond Platnumz na kuachia wimbo wake wa kwanza uliotamba sana wa “Kwetu”. Mwaka 2017, aliweka historia kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kushinda tuzo ya kimataifa ya BET Award (Viewer’s Choice: Best New International Act). Pia amefanya kolabo na wasanii wengi wakubwa kama Harmonize, Mbosso, na Alikiba. Ameshawahi kutoa albamu na EP maarufu kama Sound From Africa, Flowers, na Flowers II.

Songs, EP & Albums

Pakua na sikiliza nyimbo zake zote mpya za Audio Mpya za Bongo Flava, MP3, video, pamoja na Album na EP zake zote hapa chini. Pia unaweza kutazama orodha yote ya Nyimbo Mpya zilizotoka wiki hii kupitia Zilizovuma.