Nyimbo Mpya Wiki Hii

Mbosso Biography
Mbwana Yusuph Kilungi, anayejulikana zaidi kwa jina la kisanaa la Mbosso (au Khan), ni mmoja wa wasanii wakubwa na wenye sauti ya pekee ya muziki wa Bongo Flava, Taarab, na Mapenzi nchini Tanzania na barani Afrika. Yeye ni msanii aliye chini ya lebo maarufu ya muziki ya WCB Wasafi.
Early Life and Background
Mbosso alizaliwa tarehe 3 Oktoba 1991 katika Mkoa wa Pwani (Kibiti/Rufu) na kukulia jijini Dar es Salaam. Safari yake ya muziki ilianza kuonekana wazi alipojiunga na kundi la vijana la Yamoto Band (pamoja na Aslay, Beka Flavour, na Enock Bella), ambalo lilipata mafanikio makubwa sana kabla ya kuvunjika.
Music Career and Breakthrough
Baada ya kuvunjika kwa Yamoto Band, Mbosso alipitia kipindi kigumu cha kirejea kijijini kulima kabla ya kusainiwa rasmi na lebo ya WCB Wasafi mwaka 2018. Wimbo wake wa kwanza chini ya WCB, “Watakubali”, ulimrudisha kwa kishindo sokoni na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wanaopendwa zaidi kwa nyimbo za hisia na mapenzi. Ameshawahi kutoa albamu maarufu kama Definition of Love na EP ya Khan.
Songs, EP & Albums
Pakua na sikiliza nyimbo zake zote mpya za Bongo Flava, audio MP3, video, pamoja na Album na EP zake zote hapa chini.